Home Habari za Kitaifa MLL-TANZANIA YAZINDUA BIDHAA MPYA

MLL-TANZANIA YAZINDUA BIDHAA MPYA

0

Sekta ya ujenzi nchini imepata bidhaa mpya inayotarajiwa kuleta mapinduzi ya aina yake na kuboresha sekta ya ujenzi nchini, kipindi hiki ambacho uchumi wa Tanzania unazidi kuimarika.

Mwandishi wa TriGen Media, Joseph Mwanicheta anakuja na habari kwa kina kutoka jijini Dar es Salaam…

Newta hii ni bidhaa mpya nchini iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam mapema wiki ikitajwa kuwa mkombozi kwa makandarasi na mafundi ujenzi wa Tanzania.

Newta inatengenezwa na kampuni tanzu ya Huaxin Group; Maweni Limestone Limited (MLL-Tanzania), kampuni ambayo imepiga hatua kubwa kibiashara kwa sasa.

Haya yanajiri wakati miradi mingi ya ujenzi ikiendelea kutekelezwa huku ikihitaji bidhaa bora kama Newta katika utekelezaji wake.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Newata iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa kampuni ya Huaxin Group, Wang Jiajun, anasema utafiti wa kina umefanyika na kuja na wazo la kuzalisha bidhaa mpya itakayokidhi mahitaji katika sekta ya ujenzi.

Makamu wa Rais wa Kampuni ya Huaxin Group ambayo ni kampuni mama ya Maweni Limestone (MLL-Tanzania, Wang Jiajun (aliyevaa koti), akiongoza watendaji wengine katika uzinduzi

“Matokeo ya utafiti wetu yametupatia bidhaa ya hali ya juu katika soko la ujenzi Tanzania. Newta ni rahisi kutumia hata kwa mafundi wapya wanaoingia kazini kwa mara ya kwanza. Bidhaa hii mpya itawawezesha kufanya umaliziaji wa ujenzi vizuri,” anasema.

Sifa nyingine za bidhaa hiyo ni uimara utakaowawezesha makandarasi na wamiliki wa miradi kuokoa muda wakati wa utekelezaji wa miradi husika.

“Hii ni kwa kuwa Newta hukauka mapema na hivyo kutoa fursa kwa mafundi kuendelea na shughuli nyingine za umaliziaji,” anasema Jiajun.

Makamu huyo wa Rais wa Huaxin Group anatoa rai kwa wageni waalikwa kutumia fursa zitakazotokana na Newta yenye mwonekano mzuri utakaoifanya nyumba kuwa ya kuvutia.

Newta inazalishwa katika kiwanda kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, sambamba na bidhaa nyingine za kampuni hiyo kubwa.

Kutokana na MLL-Tanzania kuwa na miundombinu stahiki, Newta itapatikana kwa urahisi na kwa wakati katika kila kona ya Tanzania.

“Tuna imani nayo na tunatumaini kwamba Watanzania wataipokea vyema na kuthamini matokeo ya kazi nzuri iliyofanywa na uongozi wa kampuni yetu,” anasema.

Jiajun anaishukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji hivyo kuvutia wafanyabiashara wengi kuja kuwekeza Tanzania.

“Mazingira bora ya uwekezaji yamesababisha kampuni yetu ambayo ni moja ya wazalishaji wakubwa wa bidhaa za ujenzi duniani, kuja kuwekeza Tanzania.

“Kwa Tanzania, Mbali na kiwanda cha Mkuranga, Huaxin Group pia tuna kiwanda cha MLL-Tanga kilichoko mkoani Tanga,” anasema Jiajun.

Maonyesha Newta wakati wa uzinduzi wake jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MLL-Tanzania, Louis Liu, Mkuu wa kitengo cha Biashara wa Huaxin Group kimataifa, Jessica Ma, mawakala, viongozi wa serikali na wadau wengine wa sekta ya ujenzi nchini.

Huaxin Cement MLL-Tanzania, ilianza kuwekeza nchini mwaka 2019, huku kampuni yake mama, Huaxin Group ikiwa imeanzishwa mwaka 1907. Huaxin Group ni wazalishaji wakuu wa vifaa vya ujenzi nchini China ikiwa imetawanyika katika nchi 18 kupitia kampuni tanzu zaidi ya 300.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Exit mobile version