Home Habari za Kitaifa FADHILI NGAJILO AJITOSA UBUNGE IRINGA MJINI

FADHILI NGAJILO AJITOSA UBUNGE IRINGA MJINI

0

Je unaukumbuka wimbo huu nyakati za kampeni za kisiasa?Ulioimbwa na Hayati Kaptain John Komba? Ni huu ‘’sasa kumekuchaa Jogoo limewika kule Dodoma’’ akimaanisha mbio za kampeni za kisiasa kuanza kutimua vumbi’’ Maneno ya wimbo huu bado yanaishi mpaka sasa kwani kumekucha kweli.

Muonekano wa Iringa mjini ambayo Fadhili Ngajilo amepania kuwa muwakilishi wake. Picha na Trigen.

HII NI TRIGEN MEDIA

Wakati joto likipanda kila kona ya nchini tayari kwa kuanza mbio nyingine za kusaka nafasi za Udiwani,Ubunge na Urais zikiwa zimeanza huko mkoani Iringa nako moto umewaka baada ya June 13, 2025 kada wa Chama cha Mapinduzi Mkoani humo  Fadhili Ngajilo ameweka wazi nia yake ya kuwania ubunge katika jimbo hilo.Ngajilo ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Iringa ametangaza nia hiyo mbele ya waandishi wa Habari na Trigen  ikiwepo katika mkutano huo ambapo akikaririwa akisema kuwa amejipima na kuona anafaa kuliongoza jimbo hilo.

Amesema kuwa jimbo la Iringa mjini kwa sasa linahitaji mbunge ambaye ni mbunifu kutokana na uwepo wa fursa nyingi za kiuchumi zinazochagizwa na uchapakazi wa wananchi wa jimbo hilo na fursa mbali mbali zikiwemo za utalii.

Ametaja miongoni mwa sababu 10 zilizomsukuma kutia nia ya kugombea ubunge wa jimbo hilo kuwa ni  pamoja na Iringa kuhitaji mtu anayeweza kusikia  sauti za watu na kuzipeleka mbele kwa uhakika, huku akibanisha kuwa Iringa Mjini inahitaji mbunge aliyejaa uelewa wa mahitaji ya vyuo vikuu na elimu na mtu anayetambua maana ya kuweka mifumo ya burudani na michezo.

Huyu ndiye Fadhili Ngajilo mtangaza nia ya Ubunge Iringa Mjini aliahidi kuwa mwakilishi bora wa jimbo la Iringa.

Hii ni mara ya tatu kwa Fadhili Ngajilo kuingia katika mchakato wa kuwania ubunge wa jimbo la Iringa mjini ambapo alifanya hivyo mwaka 2010 na 2020 bila mafanikio

Jimbo la Iringa mjini kwa sasa linaongozwa na Mbunge Jesca Msambatavangu ambaye alishinda uchaguzi wa mwaka 2020 kutoka kwa Mchungaji Peter Msigwa aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA. Sasa kweli kumekucha huenda ni jambo la kusubiri na kuona.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Exit mobile version