Kilimo kina umuhimu mkubwa na machango mkubwa katika uchumi na ustawi wa Bara la Afrika, na kuchangia pato la taifa, ajira na usalama wa chakula. Inaajiri sehemu kubwa ya wafanyakazi, inasaidia maisha ya watu wengi, na ina jukumu muhimu katika ukuaji wa jumla wa uchumi wa bara lote.

Kutokana na umuhimu huo Kampuni ya Kilimo Roundtable Africa ya nchini Tanzania kwa kushirikiana na Uchumi Institute wameandaa kikao kazi maalum na Mashirikiano ya wadau wote walio kwenye mnyororo wa thamani wa Kilimo,ambapo mkutano huo unatarajiwa nkufanyika mjini Dodoma April 24.2025 katika hoteli ya Morena ambapo masuala mbali mbali yatajadiliwa ili kuweza kuona namna na kuweza kufanikisha malengo ya kuimarisha kilimo na ndoto za Tanzania kuilisha Afrika.

Akizungumzia mkutano huo Mkurugenzi wa Kilimo Roundtable Africa Rhoda Magoiga Mwita aliambia mtandao wa Trigen kwamba hiki kinakuwa kikao kazi cha pili kwani mwaka jana pia walifanya kikao kazi kama hiki ambapo wadau mbali mbali wa kilimo na wakulima wenyewe walipata fursa ya kupata dira halisi ya kilimo na safari ya kujiimarisha na kujitosheleza katika uzalishaji kupitia kilimo,uongezaji mnyonyoro wa thamani pamoja na kuongeza ajira kupitia kilimo.
Hata hivyo link maalum ya washiriki kuweza kuthibitisha ushiriki wao imeundwa ili kuhakikisha hakuna mkulima ama mdau wa kilimo mwenye nia ya kufika anayekosa fursa hiyo adhimu.
Hata hivyo matukio yote katika kikao kazi hicho yatarushwa mbashara na Mchongo TV ambao wamedhamiria kuhakikisha habari za kilimo na shughuli zote zihusuzo kilimo zinapewa kipaumbele kama ilivyo kwa habari nyinginezo.