Home Habari za Kitaifa Uganda kuunganisha reli na Tanzania, yaachana na mpango wa Kenya

Uganda kuunganisha reli na Tanzania, yaachana na mpango wa Kenya

0

Kwa mara nyingine ndani ya chini ya miaka 10, Serikali ya Uganda inapanga kuwekeza mabilioni ya fedha kwenye mradi unaoiunganisha na Tanzania.

Hii hapa taarifa ya Reuters kama inavyoripotiwa na mmwandishi wa kimataifa wa TriGen Media

Uganda inataka kuunganisha reli yake mpya ya kisasa (SGR) na reli inayojengwa nchini Tanzania, hatua inayotarajiwa kufungua njia mbadala ya kusafirisha nje madini muhimu kama dhahabu, shaba na madini ya chuma.

Kwa mujibu wa waraka wa serikali ulionukuliwa na Reuters, mradi huo utapunguza utegemezi wa Uganda kwa bandari ya Mombasa nchini Kenya, ambayo kwa sasa ndiyo njia kuu ya usafirishaji wa bidhaa zake kwenda kwenye soko la kimataifa.

Mradi wa reli ya kisasa (SGR) upande wa Tanzania unaendelea

Awali, kabla ya kuwekwa wazi nia ya kuunganisha SGR ya Uganda na ile ya Tanzania, Uganda ilikuwa imetangaza mpango wa kuunganisha reli yake na ile ya Kenya, wazo ambalo bado linachakatwa.

Kwa kuunganisha na mtandao wa reli wa Tanzania, Uganda itatumia bandari ya Dar es Salaam badala ya Mombasa.

“Reli hiyo mpya itaanzia mpakani mwa Tanzania, ikipita maeneo ya kusini na kusini-magharibi na kuishia katika Mji wa Mpondwe, mpakani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Uganda inapanga kuiunganganisha Tanzania na kaskazini mwa DRC kupitia SGR

“Lengo kuu la mradi huu ni kuunganisha maeneo yenye utajiri mkubwa wa madini katika nchi zote mbili — Uganda na Tanzania — na bandari ya Dar es Salaam, hivyo kupunguza muda na gharama za usafirishaji,” inasomeka sehemu ya waraka huo.

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) inatajwa kuwa mfadhili tarajiwa wa mradi, huku DRC nayo ikitarajiwa kuunganishwa baadaye.

AfDB imethibitisha kuwa inapitia ombi la kufadhili shughuli za maandalizi ya mradi.

“Benki itafadhili mradi huo kutegemeana na matokeo ya tafiti, iwapo utaonekana kuwa na uhimilivu wa kifedha,” anasema afisa wa AfDB, Epifanio Carvalho de Melo.

Tanzania imeanza usafirishaji wa shehena kwa SGR

Ndani ya muongo mmoja uliopita, Uganda ilipanga kushirikiana na Kenya kujenga bomba la kusafirishia mafuta ghafi, kabla haijabadili mawazo na kuamua kushirikiana na Tanzania.

Kwa sasa ujenzi wa mradi wa bomba hilo unaofahamika kama East African Crude Oil Pipeline Project (EACOP) upo katika hatua za mwisho za utekelezaji, ukianzia Hoima nchini Uganda hadi Chongeleni, Tanga nchini Tanzania.   

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Exit mobile version