Home Habari Kimataifa NITAUNGANISHA TAIFA,NITATIBU MAJERAHA:RAIS MYUNG

NITAUNGANISHA TAIFA,NITATIBU MAJERAHA:RAIS MYUNG

0

Saa chache tu baada ya kushinda kiti cha urais wa Korea Kusini, Lee Jae-myung aliahidi “kuwaunganisha watu” katika hotuba yake ya kuapishwa kwake siku ya Jumatano.

HII NI TRIGEN MEDIA

Lee anaingia Maadarakani wakati ambapo taifa hilo la Korea Kusini likikabiliwa na mgawanyiko mkubwa, ambao uliongezeka zaidi baada ya tamko la Rais Yoon Suk Yeol la sheria ya kijeshi iliyoleta mshituko kwa taifa zima.

“Nitaanza na kufufua uchumi na kuponya watu majereha,” aliambia hadhira katika Bunge la Kitaifa. “Bila kujali ulimuunga mkono nani katika uchaguzi huu… nitakuwa rais wa watu wote.”

Lee, ambaye aliwania nafasi hiyo kupitia chama cha kiliberali cha Democratic, alichaguliwa kwa takribani asilimia 50 ya kura zote.

Alilaumu misukosuko ya kisiasa nchini humo kutokana na “makundi ya kisiasa yasiyo na nia ya kufanyia kazi maisha ya watu”.

“Nitafanya kazi ya kuwaunganisha wananchi,” alisema na kuongeza kuwa “atakuwa rais anayemaliza siasa za migawanyiko.”

Hata hivyo alisema si kwamba atafanya mambo ya ndani tu,bali hata kusimamia vyema sera za nje.

Rais Lee ana changamoto za dharura za kigeni pia – kama vile kuendana na utawala wa mpya wa Marekani chini ya Rais Trump na kusawazisha uhusiano wake na China na kushughulika na jirani yake wa karibu zaidi Korea Kaskazini ambaye kwa muda mrefu uhusiano wao umekuwa ukiyumba.

Lee pia ameahidi kujenga “serikali inayoweza kubadilika na inayotekeleza mambo na akatangaza kwamba kikosi kazi cha dharura cha kiuchumi “kitaanzishwa mara moja”.

Historia ya Marais katika taifa hili la Korea Kusini inaanzia mwaka 1948 ambapo Rhee Syng-manmwenye mrengo wa shoro ndiye aliyekuwa  rais wa kwanza wa Jamhuri ya Korea.

Rais aliyefuata alikuwa na mrengo wa kulia ambaye  Park Chung Hee na ambaye ndiye aliyekaa muda mrefu zaidi madarakani kwani alikaa kuanzia mwaka 1961 hadi mwaka 1970.

Chini kushoto: Roh Tae-woo akiwa na mrengo wa kati kushoto yeye alichaguliwa wakati wa uchaguzi wa urais wa 1987, na kuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kwa awamu moja chini ya katiba ya kidemokrasia. Na sasa ni rais Lee Jae-myung ambaye yeye ana mrengo wa kati.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Exit mobile version