Home Habari za Kitaifa GEN-Z NA VIONGOZI WA KISIASA WAANDAMANA KENYA

GEN-Z NA VIONGOZI WA KISIASA WAANDAMANA KENYA

0

Polisi nchini Kenya wameendelea kukabiliana na waandamanaji katika maeneo kadhaa ya Jiji Kuu la Nairobi. Hata hivyo maandamano ya safari hii yamekuja na mambo mapya kwani waandamanaji wameonekana wakicheza mpira huku wengine wakirusha mawe barabarani, nao polisi wakirusha mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamaji hao.

HII NI TRIGEN MEDIA

Idadi ya Polisi wanaokabiiana na vijana imeongezeka katika barabara ya Moi, ambapo wanarusha mabomu ya kutoa machozi huku wakilazimika pia kuwamwagia maji ya rangi nyekundu inayowasha mwili.

Naye aliyekuwa Jaji Mkuu nchini Kenya David Maraga amejiunga na maandamanao ya Gen Z jijini Nairobi huku akilaani ukatili wa maafisa wa Polisi dhidi ya vijana hao waandamaji.

Maraga amekaririwa akisema Vijana hawa wana amani na kwamba watashirikiana nao kufanya maandamano ya amani. Wanataka katiba iheshimiwe, wanataka maisha ya binadamu kuheshimiwa, inasikitisha kuona vijana wamezuiwa kufanya maandamano kuelekea bungeni ,mbali na mihemko tunayoina hapa leo,hakuna ghasia za aina yoyote,”.

Jaji Mstaafu Maraga akiwa miongoni mwa waandamanaji jijini Nairobi. Picha na NMG

Katika maandamano hayo yanayodaiwa kuwa kuwakumbuka Vijana wenzao waliuawa katika maandamano yaliyofanyika awali,huku wakiwasha moto katikati ya barabara huku wakiweka mawe barabarani na matairi ya gari ambayo wameyawasha moto.

Kwa upande wake Wiper nchini Kenya Kalonzo Musyoka aliwaongoza viongozi wa upinzani jijini Nairobi kuwakumbuka vijana wa Gen Z waliofariki Juni 25, kabla ya hafla iliyopangwa ya kuweka shada la maua.

Viongozi hao wa upinzani waliandamana hadi Barabara ya Bunge kuweka shada la maua na kuwasha mishumaa kwa heshima ya waandamanaji wa Gen Z waliopoteza maisha yao wakati wa maandamano ya 2024.

Mnamo mwezi  Aprili mwaka huu, Jaji Maraga alitangaza rasmi nia yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2027 nchini Kenya.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Exit mobile version