Home Habari za Kitaifa VIJANA WA KITANZANIA WANAIPENDA AMANI NA HAWATAKUBALI CHOKOCHOKO

VIJANA WA KITANZANIA WANAIPENDA AMANI NA HAWATAKUBALI CHOKOCHOKO

0

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera, Faris Burhani, amesema kuwa vijana wa Tanzania ni watu wenye akili timamu, jambo linalowasaidia kutumia maarifa yao kwa wivu mkubwa katika kuilinda amani ya taifa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya KIJANI FIRST TIME VOTERS uliofanyika katika makao makuu ya nchi jijini Dodoma, Faris alieleza kuwa kuna baadhi ya wanaharakati kutoka nchi jirani ambao wameanza kuleta chokochoko na kutoa maneno ya dhihaka dhidi ya Serikali ya Tanzania.

Kauli hiyo aliitoa kwa niaba ya vijana wa CCM Mkoa wa Kagera, katika hafla hiyo ya uzinduzi iliyoongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Comrade Mohamed Ali Kawaida, pamoja na Baraza lake la Vijana Taifa.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Exit mobile version