Home Kimataifa MAUAJI YA RAIA 26 WA INDIA UMETIBUA UHUSIANO NA PAKISTAN

MAUAJI YA RAIA 26 WA INDIA UMETIBUA UHUSIANO NA PAKISTAN

0
Baadhi ya waandamanaji wakipinga mauaji ya watalii na waasi karibu na eneo la Pahalgam huko Kashmir,Picha na Ajit Solanki/AP

India imemtaka mwanadiplomasia wake mkuu wa Pakistan mjini New Delhi kutokana na uhusiano kati ya mataifa hayo mawili kuzorota kufuatia shambulizi la siku ya Jumanne lhuko Pahalgam na kuua watu wapatao 26.
Haya yanajiri siku moja baada ya India kuchukua hatua kadhaa dhidi ya Pakistan, ikiwa ni pamoja na kufunga mpaka wake na taifa hilo.


Shambulio hilo katika wilaya ya kusini mwa mji wa Kashmir ya Anantnag limezusha hasira kote nchini India. Hata hivyo shambulizi hilo limekuja katika kilele cha msimu wa watalii wakati huku mamia kwa maelfu ya watalii wakiwa wamejipumsha katika eneo hilo, ambalo limekumbwa na uasi wa kutumia sialaha kwa miongo mitatu hadi sasa.
Mara tu baada ya shambulio hilo, timu za polisi na askari wa kijeshi walikimbilia mahali hapo ili kuwaondoa watalii waliojeruhiwa na kuanzisha msako wa kuwasaka washambuliaji. Waziri wa Mambo ya Ndani wa India Amit Shah, pamoja na mkuu wa usalama wa nchi hiyo, walikimbilia Kashmir, wakati Waziri Mkuu Narendra Modi alikatisha ziara ya Saudi Arabia kurejea New Delhi, ambapo alifanya mkutano Jumatano asubuhi kuandaa majibu ya India.

Jambo jingine ni kwamba tukio hili limekuja huku makamu wa Rais wa Marekani JD VANCE akiwa ziarani nchini India ambapo aliwasili nchini humo tangu siku ya Jumatatu.

Vikosi vya jeshi la India vikiimarisha ulinzi karibu na eneo la utalii la Baisaran karibu na Pahalgam kusini mwa Kashmir ambako lilitokea shambulizi na kuua watu 26.

Kwa mujibu wa shirika la habari za Aljazeera ni kwamba Eneo hilo la Pahalgam, jina linalo maanisha “valley of shepherds yaani Bonde la wachungaji” huko Kashmiri, ni moja ya maeneo yanayotembelewa zaidi na watalii katika jimbo hilo ambalo lipo umbali wa kilomita 50 kutoka mji wa Srinagar.Hata hivyo Al Jazeera haijaweza kuthibitisha kwa uwazi taarifa za kundi hilo kuhusika kutekeleza shambulizi hilo.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Exit mobile version