Tuesday, June 17, 2025
spot_img

Idadi ya watu walionyongwa duniani yaongezeka

SHIRIKA la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, imesema idadi ya watu walionyongwa mwaka jana imeongezeka huku Iran, Iraq, na Saudi Arabia zikitajwa kuongoza katika kutekeleza adhabu hiyo.

Taarifa ya kila mwaka  inaonyesha kuwa  jumla ya watu 1,518 walinyongwa duniani kote mwaka 2024, ikiwa ni  sawa na ongezeko la asilimia 32 kutoka mwaka 2023.

Katibu Mkuu wa  Shirika la Amnesty International , Agnes Callamard, amesema utekelezaji wa adhabu ya kifo ni kukiuka haki za msingi za binadamu ambao haukubaliki kwa miaka ya sasa

Katika  takwimu hizi  Amnesty International  ilishindwa kujumuisha maelfu ya watu  walionyongwa nchini China  ambao wanadaiwa kuongoza kutekeleza adhabu ya kifo

Katika ripoti hiyo, Iran imenyonga watu 972, wakati Saudi Arabia iliongeza idadi ya watu waliowanyonga kwa kuwakata vichwa  kutoka 172 hadi karibu 345, na Iraq nayo ikiongezeka kutoka 16 hadi 63.

Zinazihusiana

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Ungana Nasi Kupitia

0FansLike
0FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Za hivi karibuni