Tuesday, November 4, 2025
spot_img

ISRAEL YAENDELEZA MPANGO KUITEKA GAZA

Israel imeanzisha mashambulizi mapya katika mji wa Gaza, ambao inapanga kuuteka, na kuwaondoa kwa  nguvu takribani  watu milioni moja ambapo mashambulizi hayo pia yana ambatana na ubomoaji wa kimfumo” wa nyumba za raia wa Palestina.

HII NI TRIGEN MEDIA

Hamas kwa upande wake wamemlaumu moja kwa moja Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa kupuuza jitihada za wasuluhishi wa kimataifa wanaolenga kusitishwa kwa vita hivyo huko Gaza.

Viongozi wa Dunia wameilaumu Israel kwa kupitisha  mpango wake wa upanuzi wa makazi unaoitwa E1 settlement expansion, Mpango unaolenga kumega  moja ya maeneo yanayounganisha  Ramallah na Bethlehem, huko katika Ukingo wa Magharibi eneo linalokaliwa kwa nguvu na Israel. Mashambuliz haya ya Israel siku ya jumatano yaliwaua raia 81 wa Palestina huko Gaza.

Baadhi ya Raia wa Gaza wakihama katika maeneo ya Mapigano. Picha na AFP

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA kwa mara nyingine tena limetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano huko Gaza, Na kuongeza kuwa vita hiyo imesababisha  watoto katika eneo la pwani ya Gaza kukosa masomo kwa  mwaka wa tatu hadi sasa.

“Badala ya kujifunza, watoto hutumia wakati wao kutafuta maji na chakula,” imesema taarifa ya shirika hilo iliyotolewa kupitia ukurasa wake wa X,na kuhimiza kwamba mapigano yanapaswa Kusitishwa haraka.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka kusitishwa kwa mapigano mara moja huko Gaza, huku jeshi la Israel likizidisha mashambulizi kwenye mji wa Gaza ambao linajiandaa kuuteka.

Jitihada za kimataifa zinazoendelea kuhusiana na vita vya Israel na Gaza kila uchao unazidi kuwa na utata pamoja na jitihada za usuluhishi ambazo bado hazija zaa matunda.

Zinazihusiana

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Ungana Nasi Kupitia

0FansLike
0FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Za hivi karibuni