Mkutano kati ya Rais wa Ukaine Volodymyr Zelensky na Rais wa Marekani Donald Trump unaonekana kuamsha hisia mpya kabisa ya Umoja wa Ulaya ambao kwa sasa wanaona kama mwenendo wa Trump unaweza kuvuruga kabisa mpango wao wa awali wa Ukraine kuifanya mwanachama wa NATO msimamo ambao Trump anasema ni jambo lisilowezekana Ukraine kujiunga na NATO.
Hii ni Trigen Media.
Itakumbukwa kwamba baada ya wiki iliyopita Trump kukutana na rais Putin kilichofuatia, ilikuwa ni kupanga ratiba ya kukutana na Rais Zelensky August 18 yaani siku ya jumatatu.
Msimamo uliowekwa wazi na Trump ni kwamba Ukraine haiwezi kuwa Mwanachama wa NATO hatua ambayo awali ilikuwa na ukakasi kwa Urusi kuiona Ukaine ikiwa Mwanachama wa NATO.

Lakini kwa sasa msimamo huu wa wazi wa Trump baadhi ya wachambuzi wanaona kuwa ni kama anaegemea matakwa ya Urusi zaidi na hasa ukizingatia kwamba matamshi yake yanakuja muda mfupi tu, baada ya kuonana na Rais Putin na huenda ni jambo la kusubiri na kuona Umoja wa Ulaya watachukua hatua gani kutetea msimamo wao wa awali wa kuiona Ukraine akiwa mwanachama mpya wa NATO.
Hata hivyo jambo linalo oneshwa kwamba Zelensky huenda akajikuta njiapanda katika suala zima la kwamba aegemee wapi na asiegemee,wapi linaanza kuwa gumu kwa kile anachokisimamia na hasa katika hali inayoweza kumfanya ashindwe kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja, yaani umoja wa ulaya na mawazo yao ya yeye kujiunga na NATO pamoja na msimamo wa Marekani ambayo haihitaji kumuona Ukraine akiwa mwanachama wa NATO.
Katika mkutano huu kati ya Zelensky na Trump ni kwamba atasindikizwa na viongozi wa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Finland, na Kamisheni ya Ulaya na Nato,hiyo ni ishara kwamba ameanza kubanwa mbavu.
Baadhi ya wadadisi wa masuala ya kisiasa wanaichukulia hatua hiyo kwamba ina malengo ya kutuma ujumbe kwa Trump na mshirika wake Putin ambaye kwa muda sasa amekuwa katika hali ya kutengwa na umoja wa Ulaya.
Wasi wasi mwingine mkubwa kwa Umoja wa Ulaya ni kwamba huenda Putin kupitia Trump anaweza kutimiza malengo yake kwa Ukraine, jambo ambalo wasingelipenda kuona likitokea.
Mtego mwingine kwa Ukraine ni kuhusiana na misaada ya kijeshi kutoka umoja wa Ulaya,itakuwaje ikiwa ataonekana kuegemea kwenye ushauri wa Rais Trump ambaye kwa mbaali tayari anaonekana kuwa na makubaliano ya siri na Putin.
Hata hivyo ikikumbukwe kwamba bado Ukraine inaendelea kujitia kitanzini kwani awali,walikwisha ingia makubaliano ambayo ya mikataba kuhusiana na namna ya kuheshimu mipaka ya kila upande baina yao,lakini makubaliano na mikataba hii mipya kwa sasa inaonesha kwamba huenda kukazuka mambo mapya ambayo yanaweza kuwa kinyume kabisa na makubaliano yao ya awali. Hili ni jambo la kusubiri na kuona,na Je Trump atakubaliana pia kuzungumza na Zelensky mbele ya hao wanaodai kumsindikiza Zelensky? huenda ni jambo la kusubiri na kuona.
Na hii ni Trigen Media.



                                    