Kama kuna ndoto ambayo Rais Trump angelipenda iweze kutimia ni kumalizika kwa mzozo wa Ukraine na Urusi. Na kutimia kwa ndoto hiyo kunaweza kutimiza ahadi yake na moja ya jambo ambalo lilimuongezea kura katika uchaguzi mkuu wa Marekani,pale alipojinasibu kuwa ana uwezo wa kumaliza mzozo huu kati ya Urusi na Ukraine.
Fuatilia uchambuzi huu wa Trigen Media.

Jitihada za Rais Trump katika mzozo dhidi ya Ukraine na Urusi haziwahi kuisha kwani sasa pia amekutana na Rais wa Urusi kwa mazungumzo ya faragha japo kuwa kilichokubaliwa huko bado ni siri ya mtungi,lakini hadharani akieleza kuwa wamefikia mwanzo mzuri.
Mara baada ya mkutano wake na Rais Putin ambaye amempokea kwa heshima na taadhima,Trump kupitria ukurasa wake wa Truth alikaririwa akisema kuwa mazungumzo yao yalikuwa na tija kubwa,bila kuingia kwa undani ni tija ya namna gani katika utatuzi wa mzozo wa Ukraine na Urusi.
Mara baada ya mazungumzo na Putin Rais Trump akaamua kuwa na mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Ukraine Volodymir Zelensiky na wote wawili wamekubaliana kuwa njia bora ya kumaliza vita hivyo ni kuwa na njia ya kuwa na Mkataba wa Amani”.

Kifuatacho kwa sasa katika jitihada hizi endelevu za Rais Trump na mzozo wa Ukraine na Urusi ni kukutana uso kwa macho na Rais wa Ukraine Zelensky – huko washington DC siku ya jumatatu Agosti 18,2025 kwa mazungumzo zaidi kabla ya kumrudia tena Rais Putin kwa mkutano mwingine,ikiwa ni pamoja na kuweza kulinganisha misimamo ya pande hizi mbili katika hili.
Jambo jingine Rais Trump amesisitiza juu ya umuhimu wa viongozi wa Ulaya kuwepo “katika kila hatua ya kile kinachoendelea kusaka amani ya Ukraine na Urusi.
Hatua ya Rais Putin kukutana na Trump inaonekana kuwachanganya umoja wa Ulaya na msimamo wao pamoja na vikwazo dhidi ya Putin, ambaye kwa upande wake kwa sasa huu ni ushindi na kuanza hatua ya kujitoa katika wimbi la kutengwa na mataifa ya Ulaya,ambapo Trump yeye hapa hasikii la muita swala wala la shekh anachohitaji ni kutatua mzozo huu na yeye apate ushindi na kile anacho kisaka baada ya mzozo.
Baadhi ya wachambuzi wa siasa wanaona hapa nafasi ya Zelensky kuamua kwa maslahi ya taifa lake yanaendelea kubanwa na kwamba itafika wakati atalazimika kuamua kwa kuyatoa baadhi ya maslahi ya taifa lake,na hasa tukirejea msimamo wa Rais Trump pale anapotaka lake liwe.
HII NI TRIGEN MEDIA



