Thursday, January 22, 2026
spot_img

NYOTA WA LIVERPOOL DIOGO JOTA AFARIKI DUNIA

Mmoja kati ya washambuliaji mahiri wa mabingwa wa England, Diogo Jota amefariki dunia kwa ajali ya gari.

Hii hapa taarifa ya awali kutoka Hispania kama ilivyoripotiwa na vyanzo mbalimbali vya habari na kufika TriGen media.

Jota, raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 28 ni amefariki dunia wiki mbili tu baada ya harusi yake.

Diogo Jota akiwa uwanjani

Kifo cha mshambuliaji huyo aliyekuwa na mafanikio makubwa akiwa na Liverpool, kimetokana na ajali ya gari iliyotokea nchini Hispania.

Inaripotiwa kuwa Jota alikuwa akisafiri na mdogo wake, André (26), ambaye naye ni mwanasoka.

Ajali hiyo ilitokea Jimbo la Zamora, Hispania katika barabara ya A-52.

Taasisi mbalimbli zinazotoa huduma za dharura katika eneo la Castilla y León, zimethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

“Taarifa zinasema chumba cha operesheni cha 1-1-2 Castilla y León ilipokea simu kadhaa zikiripoti ajali ya gari iliyotokea kilomita 65 kwenye Barabara ya A-52, Manispaa ya Cernadilla, Zamora.

“Kwamba gari moja liliripotiwa kuhusika katika ajali hiyo na kuwaka moto.

Diogo Jota akishangilia moja ya mabao aliyoifungia Liverpool

“Huduma ya dharura ya 1-1-2 iliarifu Kikosi cha Usalama Barabarani cha Zamora, Kikosi cha Zimamoto, na Kituo cha Uratibu wa Dharura cha Sacyl (CCU) kuhusu ajali hiyo.

“Kutoka hapo, Kitengo cha Dharura ya Matibabu (UME) na wataalamu wa matibabu wa huduma ya afya ya msingi kutoka Kituo cha Afya cha Mombuey walitumwa eneo la tukio, ambapo walithibitisha vifo vya watu wawili papo hapo,” zinasema taarifa hizo.

Mabaki ya gari aina ya Lamborghini ililokuwa likitumiwa na Diogo Jota na mdogo wake, Andre.

Taarifa zaidi zitafuata…

Zinazihusiana

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Ungana Nasi Kupitia

0FansLike
0FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Za hivi karibuni