Thursday, January 22, 2026
spot_img

NYUKLIA KUCHANGIA UMEME GRIDI YA TAIFA

Katika harakati za serikali kukabiliana na ongezeko la viwanda sambamba na kukua kwa matumizi ya umeme nchini, mipango inaendelea ili kuanza kuzalisha umeme kwa kutumia bguvu za nyuklia.

Taarifa iliyoandaliwa na Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati na kuifikia TriGen Media inaeleza kwa undani…

Akizungumza jijini Kigali, Rwanda katika mkutano kuhusu masuala ya nyuklia barani Afrika, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko, amesema hivi karibuni Tanzania itaanza kuzalisha umeme wa nyuklia.

“Serikali imeiagiza Wizara ya Nishati chini ya uongozi wangu kuhakikisha kwamba umeme utakaozalishwa unajumuishwa katika Gridi ya Taifa,” anasema Dk. Biteko.

Anasema mikakati inaendelea ili kufikia azma ya serikali ya kuzalisha umeme wa nyuklia; nishati yenye unafuu wa gharama kulinganisha na vyanzo vingine huku pia ikilinda mazingira.

Baadhiya viongozi wa mataifa mbalimbali ya Afrika wakiwa Kigali, Rwanda kuhudhuria mkutano ya nyukilia barani Afrika.

Anasema mwezi uliopita Tanzania iliandaa warsha kutoa uelewa kwa wadau wa masuala ya nyuklia ikiwa na kuanzisha taasisi itakayoratibu na kusimamia shughuli za nyuklia.

“Serikali itahakikisha kunakuwapo mazingira mazuri ya uzalishaji wa nishati kwa kutumia nyuklia kwa kutunga sera thabiti na kuanzisha mifumo ya sheria na udhibiti kusimamia raslimali ya nyuklia na uzalishaji wa umeme,” anasema.

Tayari Tanzania ina nyaraka zinazoiangazia nyuklia kama rasilimali ya msingi kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya nishati ya baadae.

Nyaraka hizo ni Sera ya Taifa ya Nishati, Mkakati wa Nishati Jadidifu na Sera ya Maendeleo ya Madini.

Anasema lengo la Tanzania ni kuimarisha Sera ya Teknolojia ya Nyuklia ya mwaka 2013 kuakisi maendeleo ya hivi karibuni sambamba na kufuata viwango vya kimataifa.

Akifungua Mkutano huo, Waziri Mkuu wa Rwanda, Dk. Edward Ngirente, amesema ili kufikia Mpango wa Maendeleo wa Rwanda wa mwaka 2050 wa kuwa nchi ya kipato cha juu, wanahitaji kuwa na uzalishaji wa umeme kwa kiasi kikubwa.

Baadhi ya Washiriki wa mkutano wa masuala ya nyuklia Afrika,

“Rwanda tumeamua kuzalisha umeme wa nyuklia kwa kuwa ni salama na wa uhakika na hauhitaji mvua, ili kuharakisha maendeleo,” amesema.

Waziri Mkuu wa Niger, Ali Mahamane Lamine Zeine, amesema nchi yake ina vyanzo vingi vya nishati na imezindua mpango wake wa nyuklia kutokana na manufaa makubwa yaliyomo katika nishati hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mionzi ya Atomiki Rwanda, Dk. Lassina Zerbo, amesema Rwanda ipo katika hatua za mwisho kuanzisha vinu vya nyuklia vya kuzalisha umeme.

Mkutano huo umejumuisha wadau wa nishati kutoka ndani na nje ya Afrika wenye lengo la kuharakisha matumizi ya nyuklia kwa kutumia teknolojia ya kisasa na kuleta mabadiliko ya nishati Afrika.

Zinazihusiana

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Ungana Nasi Kupitia

0FansLike
0FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Za hivi karibuni