Thursday, January 22, 2026
spot_img

KABUKO AJITOSA UBUNGE MUHAMBWE

KABUKO AJITOSA UBUNGE MUHAMBWE

Baada ya kufanya kazi nzuri za kusimamia maendeleo wilayani Busega, Simiyu na kukubalika kwa wananchi, hatimaye Anderson Njiginya Kabuko, anaomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea ubunge Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma.

Taarifa kwa kina inaletwa kwako na mwandishi wa TriGen Media, Ruja Masawa

Kabuko alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega eneo alilolifanyia kazi ya kutuka kwa kipindi alichopewa dhamana hiyo na Serikali.

Kada wa CCM, Anderson Njiginya Kabuko

Baadaye akawa Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi (HPMU) Mkoa wa Manyara nafasi nyingine aliyoitendea haki kiasi cha kupachikwa jina la ‘Mchungaji’ kutokana na kutekeleza majukumu yake kwa weledi wa hali ya juu.

Akizungumza na TriGen Media kabla ya kurejesha fomu, mtia nia huyo anaahidi kuwa karibu na watu wote, hususan wanyonge.

“Kokote alikopita kikazi amekuwa hivyo. Yeye hushirikiana na wananchi kubuni na kuibua mawazo ya miradi ya maendeleo kwa manufaa ya taifa,” anasema mkazi mmoja jimboni hapo.

TriGen Media inafahamu kwamba baadhi ya wananchi wapenda maendeleo wa Jimbo la Muhambwe ndio wamemshawishi na kumwomba atie nia ya kuwatumikia iwapo ataridhiwa na CCM; wakiahidi kumuunga mkono kwa ari na mali.

Alipoulizwa atawafanyia nini wananchi iwapo watampa nafasi hiyo, Anderson Njiginya Kabuko anasema kwa sasa hawezi kusema lolote.

Zinazihusiana

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Ungana Nasi Kupitia

0FansLike
0FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Za hivi karibuni