Monday, December 15, 2025
spot_img

PATA GAWIO SERIKALINI HUKU UKIKUZA MTAJI

Wataalamu wa ‘Uwekezaji wa Pamoja’ wanasema kwamba zipo njia salama na za kuaminika za kuwekeza fedha zako huku ukipata faida mara mbili.

Hii hapa habari kwa undani kutoka kwa mtaalamu wa masuala ya kifedha na uwekezaji wa Kampuni ya UTT AMIS, Daud Mbaga, alipozungumza na TriGen Media

Ulimwengu wa fedha umejaa mabadiliko ya mara kwa mara, hivyo ni muhimu kutafuta njia salama na za kuaminika za kuwekeza fedha zako.

‘Bond Fund’, (Mfuko wa Hati Fungani) ya kampuni ya serikali iliyo chini ya Wizara ya Fedha, UTT AMIS, imejipambanua kama mojawapo ya chombo bora kabisa kwa wale wanaotafuta usalama wa mtaji, kukuza mtaji, huku wakipata gawio kila mwezi au kila miezi sita kutokana na matakwa yao.

Bond Fund ni mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja unaokusanya fedha kutoka kwa wawekezaji mbalimbali na kuziwekeza katika hatifungani za serikali za muda mfupi, muda mrefu, na kwenye dhamana mbalimbali.

Ofisa wa UTT AMIS, Rahim Mwanga, akitoa elimu ya uwekezaji kwa wakulima, wafugaji na wajasiriamali wadogo mkoani Kilimanjaro.

Uwekezaji katika maeneo haya unaufanya uwekezaji huu uwe tulivu na wenye hatari na athari ndogo kwa mwekezaji, ukimwezesha kupata kipato endelevu huku thamani ya mtaji wake ikikua.

Faida za kuwekeza kwenye mfuko huu ni mapato ya kila mwezi au kila miezi sita huku mtaji wa mwekezaji ukikua.

Kupitia uwekezaji katika hatifungani, mfuko huu huingiza mapato ya riba yanayogawiwa kwa wawekezaji kila mara.

Hili ni suluhisho bora kwa wastaafu, wakulima, wafanya biashara na mtu yeyote anayepata kipato kikubwa kwa msimu au mara moja huku akisubiria kipato kingine msimu mwingine, au taasisi zinazotafuta kipato cha mara kwa mara na cha uhakika.

Tofauti na hisa, mfuko huu ‘hauweki mayai yote kwenye kikapu kimoja’, hivyo kupunguza athari za kiuwekezaji.

Bond Fund huzingatia uwekezaji wenye utulivu. Uwekezaji wake mkubwa uko kwenye hatifungani za serikali, jambo linalomaanisha usalama mkubwa wa fedha za wawekezaji.

Mfuko unasimamiwa na timu ya wataalamu wa fedha waliobobea, wanaofuatilia masoko, mwelekeo wa viwango vya riba na fursa bora za uwekezaji ili kuhakikisha wawekezaji wanapata matokeo chanya.


Huwezi kuamini, unaweza kuanza kuwekeza kwa kiasi kidogo sana, kuanzia Sh 10,000 tu. Hii inatoa nafasi kwa Mtanzania yeyote, kutoka kwa mama wa nyumbani hadi mfanyabiashara, kushiriki na kuwa sehemu ya uwekezaji.

Unaendelea kuwekeza kuanzia Sh 5,000. Hakuna kikomo cha juu cha uwekezaji kwa kuanzia au kuendeleea kuwekeza.

UTT AMIS inahakikisha kuwa unaweza kuongeza au kuondoa uwekezaji wako wakati wowote, bila usumbufu. Pia hupata ripoti za thamani ya uwekezaji (NAV) kila siku, pamoja na taarifa zako zote za kiuwekezaji sio kificho (au siri), utazipata pale unazipohitaji.

Wawekezaji wa mfuko huu ni raia wa ndani na nje, wafanyakazi, wafanyabishara, wakulima, wazazi, vikundi, SACCOS na walezi. Kwa maneno mengine ni kwa kila mwenye mahitaji na kila mwenye kuweza.

Bond Fund ya UTT AMIS imeonyesha kuwa na matokeo chanya na ya kudumu, hata wakati masoko yanapita katika changamoto.

Kwa kuzingatia mwelekeo thabiti wa uchumi wa Tanzania na usalama wa hati fungani za serikali, mfuko huu unaendelea kuwa kitega uchumi cha kuaminika na chenye tija kwa muda mrefu.

UTT AMIS Bond Fund umeonesha ukuaji thabiti na wa kuvutia tangu kuanzishwa kwake.

Thamani ya kipande (unit price) imeongezeka kutoka Sh 100 Oktoba 2019 hadi takriban Sh 121 ilipofika Juni 24, 2025.

Ukuaji huu unadhihirisha ustahimilivu wa mfuko na uwezo wake wa kulinda na kukuza mtaji wa wawekezaji hata katika mazingira ya kiuchumi yenye changamoto.

Mbali na ongezeko la thamani ya vipande, mfuko umekuwa ukitoa gawio la wastani wa asilimia 12 kwa mwaka, ambalo linatolewa kwa asilimia 1 kila mwezi.

Zaidi ya hayo, kila baada ya miezi sita, zaidi ya asilimia 6 huwa imeshatolewa kama gawio la mapato kwa wawekezaji, na kiasi kilichozidi kimeongezewa moja kwa moja kwenye mtaji wa mwekezaji.

Hii inamaanisha kwamba wawekezaji wanapata faida mara mbili; gawio la moja kwa moja la mapato na ongezeko la thamani ya uwekezaji wao.

Kwa ujumla, Bond Fund ni chombo bora kwa mwekezaji anayetafuta mapato ya uhakika kila mwezi pamoja na ukuaji wa mtaji kwa muda mrefu, bila hatari kubwa. Uwazi, ukwasi na ufanisi wake katika usimamizi vinaendelea kuufanya kuwa chaguo bora kwa watu binafsi, vikundi vya kifedha na taasisi mbalimbali nchini.

Tembelea tawi lolote la UTT AMIS au wakala aliyeidhinishwa, jaza fomu ya uanachama, na anza safari yako ya uwekezaji.

Utapokea cheti cha uwekezaji, taarifa zako binafsi, na msaada kutoka kwa wataalamu wa UTT, pia tembelea CRDB, na hata kwa madalali wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE).

Wasiliana na Ofisa wa UTT AMIS, Daud Mbaga kupitia namba +255712625310

Zinazihusiana

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Ungana Nasi Kupitia

0FansLike
0FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Za hivi karibuni