Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko, amewasili jijini Kigali, Rwanda kushiriki katika mkutano unaohusu masuala ya nyuklia barani Afrika.
Hii hapa taarifa kutoka Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kama inavyoriporiwa na TriGen Media
Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kuanzia leo, Juni 30 hadi Julai 1, 2025 ukijumuisha wadau wa nishati kutoka ndani na nje ya Afrika.
Lengo la mkutano ni kuharakisha matumizi ya nyuklia kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuleta mabadiliko ya nishati Afrika.

Pamoja na ushiriki wake, Dk. Biteko anatarajiwa kufungua mjadala wenye mada ya ‘Nishati Afrika na Utashi wa Kisiasa’.
Akiwa huko, Dk. Biteko ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba na Mkurugenzi wa Tume ya Mionzi ya Atomiki, Profesa Najat Mohamed.
Alipowasili nchini Rwanda, Dk. Biteko amepokelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uchukuzi wa Rwanda, Olivier Kabera.



