KATIKA hali inayoashiria bado hali si shwari katika vita vya Israel na Iran-hatimaye taifa la Tanzania limewarejesha baashi ya raia wake waliokuwa Israel kuhofia hali ya usalama kutokana na mapigano yanayoendelea dhidi ya Iran.


Kwa undani fuatilia ripoti hii ya Trigen Media
Mataifa yaliyo mengi duniani yalichukua hatua ya kuwaondoa Raia wake kwa kile kilichoelezwa kuwa ni hali ya hatari kwao kufuatia vita kati ya Israel na Iran ambavyo vimeendelea kwa zaidi ya siku 10 hadi sasa.

Hata hivyo pamoja na Rais Trump kukaririwa akisema kuwa vita imesitishwa lakini bado hali ni tete na lolote lawesa kutokea kwa pande hizo mbili.
Kati ya watanzania waliorejeshwa Baadhi yao ni wale waliokuwa wakifanya kazi- wanafunzi, na na wale waliokwenda kwaajili ya matibabu.
Wakizungumza huku wakisitasita kutokana na khofu, Hanifa Rashid Abass na Amina Soud waliorejea nyumbani wakitokea nchini Israel wanaelezea wasiwasi waliokuwa nao katika kipindi kigumu cha vita.
Mataifa haya mawili yanayopigana ni rafiki wa Tanzania na kumekuwa na mwingiliano mkubwa katika nyanja mbali mbali kama vile za kijamii-kichumi na matibabu.



