Tuesday, November 4, 2025
spot_img

BETWAY YAZINDUA ‘AVIATOR LEGENDS’ TANZANIA

Mashindano ya kwanza ya ‘Aviator Legends’ yamezinduliwa jijii Dar es Salaam yakitarajiwa kutoa fursa kwa Watanzania kuupima ujuzi na ujasiri wao.

Fuatana na Mwandishi wa TriGen Media wa masuala ya michezo ya kubahatisha kwa undani wa habari hii…

Hii ni mara ya kwanza kwa kampuni inayokubalika kuwa kinara na mvumbuzi wa kimataifa katika tasnia ya michezo ya kubashiri mtandaoni, Betway, kuleta mchezo huo Tanzania.

“NI shindano la kusisimia linawakaribisha watu wote kujaribu ujuzi, ujasiri na muda sahihi katika kurusha kindege cha Aviator,” inasema taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam, Juni 23, 2025.

Aviator Legends yanatarajiwa kuwa tukio kubwa zaidi la mchezo wa ‘crash’ kwa mwaka huu likitoa nafasi kwa Watanzania kokote waliko kushindania zawadi kubwa, miruko ya bure kila siku na nafasi ya kutangazwa kuwa ‘Aviator Legend 2025’.

“Tangu Juni 2, 2025 hadi Juni 30, 2025 washiriki waliojisajili na Betway kupitia www.betway.co.tz wamekuwa wakishiriki. Ifahamike kwamba jukwaa pekee ni Betway,” inasema taarifa hiyo.

Zawadi kwa mshindi wa kwanza ni Sh 57,500,000 sambamba na miruko ya bure kila siku na: “Washiriki wanapaswa kucheza ‘Aviator’ kwa dau la kuanzia Sh 400 kwa kipindi chote cha mwezi huu. Rusha kindege mara nyingi kisha ‘cashout’ kujikusanyia pointi za ushindi.”

Taarifa inafafanua kwamba kadri kindege kinavyoruka kwa muda mrefu, ndivyo pointi za ushindi zinavyoongezeka; lakini kuchelewa ‘ku-cashout’ kunapoteza pointi zinazohesabiwa kuzingatia viwango vya ‘multiplier’ na uthibiti wa mchezaji.

Washiriki wanane wa juu wataingia kwenye fainali kubwa itakayofanyika Dar es Salaam na kuwa katika nafasi ya kushinda zawadi ya juu; Sh 57,500,000 na kuwa ‘Aviator Legend’.

Wawakilishi wa Kampuni ya Betway wakitoa maelezo Kwa watu mbalimbali kuhusu mashindano ya Aviator Legends Jijini Dar es Salaam.

“Tunataka kuleta uzoefu wa kipekee kwa kuzindua shindano litakalohamasisha watu kushiriki na kukuza ushindani kati yao,” Calvin Mhina, Meneja Masoko wa Betway, ameiambia TriGen Media.

Mchezo huu uliotegenezwa na SPRIBE umekuwa maarufu nchini kutokana na kueleweka kirahisi na kutoa fursa kubwa ya ushindi.

Giorgi Tsutskiridze, Ofisa Mkuu wa Biashara SPRIBE, anasema: “Aviator imebadilisha dhana ya michezo ya ‘crash’, ni mchezo wa kuvutia.

“Ushirikiano wetu na Betway katika kuzindua mashindano haya ni hatua muhimu ya kufikisha burudani kwa watu wengi zaidi.

“Hapa hatuzungumzii zawadi pekee, bali pia kujenga jumuiya ya Watanzania wanaothubutu kuvuka mipaka na kufuata safari bora zaidi.”

Anasema kwa kutumia jukwaa thabiti na linaloaminika la Betway, mashindano ya ‘Aviator Legends’ yanatoa uzoefu wa kipekee kwa wachezaji wakongwe na wapya.

“Bila kujali kuwa wewe ni mchezaji wa kawaida au mwenye dau kubwa, hii ni nafasi yako kuchana anga na kuibuka mshindi,” anasema.

Zinazihusiana

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Ungana Nasi Kupitia

0FansLike
0FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Za hivi karibuni