Tuesday, June 17, 2025
spot_img

JUVENTUS MWANDISHI NA NDOTO YA UDIWANI KIBIMBA NGARA

Aliyekuwa Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa Radio Kwizera FM ya Ngara, Juventus Juvenary Illambona maarufu kama Juveilla, hatimaye amejitosa katika siasa na kutangaza kuwania  rasmi Udiwani wa Kata ya Kibimba, wilayani Ngara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

‎‎Illambona aliieleza Trigen kwamba  amefikia uamuzi huo baada ya tafakari ya kina, akilenga kuleta maendeleo kupitia uzoefu wake katika mawasiliano na utetezi wa jamii.

Mwandishi wa Habari na Mtangazaji Juventus Juvenal Illambona akiwa katika kazi yake ya utangazaji Radio Kwizera.

‎‎Miongoni mwa vipaumbele vyake ni: Pamoja na Kuboresha miundombinu ya barabara, maji na umeme,

‎‎Kuweka utawala wa uwazi na ushirikishwaji wa wananchi, Uwezeshaji wa vijana, wanawake na walemavuKukuza michezo na sanaa,

‎‎Kutumia rasilimali kama mto Ruvubu na uwanja wa ndege wa Ruganzo kwa maendeleo ya kiuchumi.

Mwandishi Juventus Juvinal na ndoto yake mpya ya kuwatumia wa Kibimba.

‎‎Amesema atachukua fomu ya kugombea tarehe 28 Juni 2025, na kuomba wananchi wa Kibimba na watu wenye mapenzi mema kumuunga mkono katika safari yake ya kisiasa.

Zinazihusiana

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Ungana Nasi Kupitia

0FansLike
0FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Za hivi karibuni