Tuesday, June 17, 2025
spot_img

IRAN YAISHAMBULIA ISRAEL KUJIBU MAPIGO

Iran imeishambulia Israel ikiwa ni hatua ya kujibu mashambulizi ya awali yaliyofanywa na Israel dhidi ya Iran.
Vyombo vya Habari vya Iran vimearifu kuwa ndege mbili za kivita za Israel zimeshambuliwa.
Kwa undani fuatilia taarifa ya Tigen Media

Kiongozi wa Iran Ayatollah Khamenei ambaye aliahidi kuwa Israel italipa gharama kwa kuishambulia Iran
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Magari ya dharula ya Israel yameonekana yakipelekwa katika eneo la yaliyopigwa ili kutoa msaada. Iran imeipa jina Operasheni hiyo la “True Promise 3”.
Hatua hii inakuja ambapo awali kiongozi wa mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ameitishia Israel kwamba itapata adhabu kali.

Awali Waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi, amesema mashambulizi ya anga ya Israel nchini humo yalichukuliwa na Iran kuwa tangazo la vita.
Wimbi la mashambulizi ya anga kati ya Israel na Iran limeendelea kuibua hofu duniani, huku mashirika ya ndege yakibadili njia zao na masoko ya mafuta na hisa zikiyumba.

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, IAEA, Rafael Grossi ameonya kuwa mashambulizi dhidi ya vituo vya nyuklia yanaweza kuwa na madhara makubwa.

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, IAEA, Rafael Grossi (Picha: Kaname Muto/Yomiuri Shimbun/AP )Images/picture alliance

Grossi amesema yuko kusafiri kwenda Iran haraka iwezekanavyo kutathmini hali baada ya kituo kikubwa cha nyuklia cha Natanz kushambuliwa.
Ameongeza kuwa hadi sasa hakuna ongezeko la mionzi lililoripotiwa, huku vituo vya Fordow na Esfahan vikiripotiwa kuwa salama.

Zinazihusiana

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Ungana Nasi Kupitia

0FansLike
0FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Za hivi karibuni