Miili ya watu 100 imepatikana kutokana na ajali ya ndege ya shirika la ndege la Air India kuanguka muda mfupi baada ya kuruka wakati ikielekea London ikiwa na abiria 242 ikiwa imepaa dakika chache kutoka mji wa magharibi mwa India wa Ahmedabad siku ya Alhamis
HII NI TRIGEN MEDIA

Ajali hii imethibitishwa na taarifa za shirika hilo la ndege na Polisi wa taifa hilo, bila kuweka wazi iwapo kulikuwa na maafa.
Ndege hiyo ilikuwa inaelekea uwanja wa ndege wa Gatwick nchini Uingereza na maafisa wa Polisi wanasema imeanguka katika eneo la makaazi ya watu karibu na eneo la uwanja huo wa ndege.
Mtandao wa kufuatilia safari za ndege wa Flightradar24 umesema ndege hiyo ilikuwa aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, mojawapo ya ndege za kisasa kabisa zinazotumika zaidi kwa sasa.
Hata hivyo taarifa zaidi zinatarajiwa kutolewa na kwamba huenda hata idadi ya vifo inaweza kuongezeka.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ameelezea kusistushwa kwake na taarifa hizo za ajali hiyo ya ajali ya ndege.
“Ajali ya Ahmedabad imetushtua na kutuhuzunisha. Haielezeki jins inavyovunja moyo, alisema Modi katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Watu waondolewa kwa haraka na kukimbizwa kwenye ambyulensi
Jitihada za uongoaji zimeonekana bayana baada ya Televisheni nchini humo kuonyesha ndege hiyo wakati ilipokuwa ikipaa juu ya eneo la makazi ya watu kisha ikaanza kupoteza uelekeo kabla ya kuzuka kwa moto mkubwa ulioonekana angani kutoka eneo hilo lenye nyumba za watu.
Baadhi ya video zimeonyesha watu wakiondolewa eneo la tukio na vitanda vya magurudumu na kupelekwa kwenye magari ya dharula.
Kulingana na kituo cha kuongoza ndege katika uwanja wa ndege wa Ahmedabad, ndege hiyo ilipaa mwendo wa saa saba na dakika thelathini na tisa kutoka barabara ya ndege ya nambari 23 na dakika chache mawasiliano ya simu kuashiria dharura yakafanyika kutoka ndani ya ndege hiyo.
Ajali hii ya ndege inatokea baada ya ukimya wa muda mrefu wa ajali za ndege nchini India ambapo mara ya mwisho ajali ya ndege ilitokea mwaka 2020 ambayo ilihusisha ndege ya shirika la Air India Express na watu 21 walifariki dunia.
HII NI TRIGEN