Je waijua Opesheni Malaam iliyoendeshwa na Ukraine huko Urus? Inaitwa Operesheni ya Spider ambayo tangu vita vya Ukraine na Urusi vianze imeandika historia ya kipekee kuwahi kutokea Urus kushambuliwa hivyo tena ndanai ya ardhi yake,kutokana na kile kinachotajwa kuwa Intelijensia imara.
Hii ni Trigen Media

Huku mazungumzo ya kusaka suluhu ya vita vya Ukraine na Urus yakiendelea huko Instanbul Uturuk,majeshi ya Ukraine yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza mpango wake wa operesheni ijulikanayo kama Spider Web ambayo wameiandaa ndani ya miezi 18.
Dunia ambayo kila uchao ilizoea kusikia Ukraine akishambuliwa ameshangazwa na ufanisi mkubwa wa Ukraine kuweza kuandaa misheni hiyo na kuifanikisha.

Mashambulizi hayo yalilenga katika kambi za anga za Urusi na yamesababisha uharibifu wa dola za kimarekani bilioni 7,lakini ni wazi kwamba “Operesheni ya Spider Web” ni ya aina yake katika historia ya vita hivi.
Raia wa Ukraine wanalinganisha mashambulizi hayo na mafanikio mengine ya kijeshi tangu uvamizi wa Urusi, ikiwa ni pamoja na kuizamisha manowari ya Urusi ya Moskva katika Bahari Nyeusi, na kulipua Daraja la Kerch, mwaka 2022, pamoja na shambulio la kombora lililolenga bandari ya Sevastopol mwaka uliofuata.
Kwa mujibu wa shirika la Ujasusi la Ukraine ni kwamba mpango huo ulikuwa hivi,ndege nyingi ndogo zisizo na rubani ziliingizwa nchini Urusi kinyemela, zikihifadhiwa katika sehemu maalum ndani ya malori ya mizigo, na kupelekwa maeneo manne tofauti, maelfu ya maili, na kisha kurushwa kuelekea katika kambi za karibu za anga,huku intelijensia za kijeshi za Urus zikiwa hazijui.
Shambulizi hilo lilifanikiwa kuzipiga ndege 40 za Urus kati ya ndege 120,haya ni mageuzi makubwa ya upepo wa vita vya Ukraine na Urus.
Mashambulizi haya ni fumbo jingine kwa mazungumzo yanayoendelea huko Instanbul Uturuki,na je yatarudi nyuma ama yatasonga mbele?na Marekani aliyeanza kusua sua katika kuisaidia Ukraine sasa atafanya nini?
Ni jambo la kusubiri na kuona hii ni TRIGEN MEDIA.Kuwa wa kwanza kupata habari mpya kwa kusubscribe channel hii.