Tuesday, June 17, 2025
spot_img

KAMANDA MKONDA AWAFUNDA MADEREVA WA TANZANIA

Pamoja na uwepo wa sababu mbalimbali za ajali barabarani madereva nao ni moja ya chanzo na wanadhamana kubwa kuhakikisha usalama wa abiria na vyombo vyao vya usafiri lakini pia hata usalama wa wao wenyewe.

Kutokana na ukweli huo Kikosi cha Uslaama barabarani nchini Tanzania kinaona suala la elimu kwa madereva ni hatua muhimu na inayoweza kusaidia kupunguza ajali barabarani na pia kuweza usalama wa wageni wakiwemo watalii husasani ni katika msimu wa utalii yaani (high season) japo kuwa hilo ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku kuhakikisha hakuna ajali.

Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha limewakutanisha zaidi ya madereva 800 wanaobeba watalii kwa ajili ya kuwapatia mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo katika utoaji huduma hiyo muhimu.

Akifungua mafunzo hayo Mei 30 mwaka huu Mkoani humo, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP William Mkonda alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwakumbusha madereva hao sheria na kanuni mbalimbali za usalama barabarani pamoja na kujadiliana changamoto wanazokumbana nazo barabarani ili kuona namna bora ya kuzitatua.

SACP Mkonda alibainisha kuwa Madereva wanaobeba watalii ni watu wa muhimu sana katika kuhakikisha usalama wa wageni kwani endapo wataendesha magari kwa kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani itasababisha kuaminiwa na kuitangaza vyema Nchi ya Tanzania na hatimaye idadi kusababisha ongezeko la watalii na wageni wengine ambao ni muhimu kwa ustawi wa taifa.

Aliwasisitiza madereva hao kuhakikisha wanatii na kufuata sheria za usalama barabarani kwa kukosoana, kuelimishana na kuonyana pindi wanapoendesha vyombo hivyo vya moto kwani itasababisha kupunguza au kumaliza ajali zisizokuwa na ulazima barabarani.

Mwenyekiti wa Waendesha Watalii Nchini (TTGA) Bw. Lembrisi Moses kwa upande wake alisema madereva hao 800 wameshiriki katika mafunzo hayo ambapo alieeleza kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kuwakumbusha wajibu wao wa kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwemo alama za barabarani, kuzingatia mwendo sahihi.

Mmoja wa madereva Usia Israel alisema kupitia mafunzo hayo amekumbushwa namna ya kuwa na udereva wa kujihami pindi awapo barabarani ambapo inasaidia kupunguza kero au ajali za barabarani ambazo zinaepukika na kuwataka madereva wenzake kuwa na udereva wa kujihami pindi wawapo barabarani.

Mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani katika kuyafikia makundi mbalimbali katika jamii kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusiana na sheria mbalimbali za usalama barabarani pamoja na mifumo mipya ya Jeshi la Polisi katika kuwahudumia wananchi.

Wito huo umetolewa leo na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP William Mkonda wakati alipotembelea Chuo cha Ufundi Arusha kwa ajili ya kuona namna ambavyo chuo hicho kinaendesha mafunzo ya udereva pamoja na watoa huduma ya mabasi ya abiria.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP William Mkonda wakati alipotembelea Chuo cha Ufundi Arusha

Kamanda Mkonda amesema Jeshi la Polisi linaowajibu wa kuvisimamia na kuvikagua vyuo vinavyoendesha mafunzo ya udereva hapa Nchini kwa ajili ya kuona ubora wa elimu inayotolewa na mitaala inayofundishwa kama inatija katika kutoa madereva makini na wanaozingatia sheria za usalama barabarani.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP William Mkonda alipotembelea Chuo cha Ufundi huko Mkoani Arusha

SACP Mkonda amepongeza uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha kwa namna ambavyo kimeimarisha miundombinu ya ufundishaji hususani ya udereva kwa kuwa na vifaa vya vya kisasa na kuwataka kusimamia mafunzo hayo vyema ili kuendelea kupata madereva wenye tija ambapo itasaidia kupunguza ajali za barabarani.

Katika hatua nyingine Kamanda Mkonda ametoa onyo kwa baadhi ya wamiliki wa mabasi na madereva kuacha tabia kujaza abiria kupita kiasi katika msimu huu ambao shule zinaenda kufungwa kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika.

Zinazihusiana

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Ungana Nasi Kupitia

0FansLike
0FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Za hivi karibuni