Matumaini ya klabu ya Simba kuwa ya kwanza kuleta ubingwa wa Afrika nchini, yezimwa leo hii Visiwani Zanzibar, baada ya kuambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya RS Berkane ya Morocco katika mechi ya mkondo wa pili ya fainali ya michuano ya Kombe la Shirikosho la Kandanda Afrika.
Simba waliingia katika pambano hilo wakiwa nyuma kwa magoli mawili ambayo walifungwa katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyofanyika Morocco, na walikuwa na matumaini makubwa ya kupindua meza ili kuandika historia mpya katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
Wakiwa wanahitajika kupata ushindi wa bao 3-0 ili kutwaa kombe hilo, Simba walianza pambano hilo kwa kasi na kujipatia bao la kuongoza kunako dakika ya 17, lililowekwa kimiani na Joshua Mutale (Budo), kufuatia kazi nzuri iliyokuwa imefanywa na Ellie Mpanzu aliyewatoka mabeki kadhaa wa Berkane kabla ya kumimina krosi iliyomkuta mfungaji.
Bao hilo lilidumu hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika na kipindi cha pili kilipoanza, Simba walianza kwa kasi kubwa wakitaka kupata mabao zaidi, lakini harakati zao zikaingia dosari baada ya kiungo wake mkabaji Yusuph Kagoma, kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kuwalazimu wenyeji kucheza pungufu kwa muda mwingi wa kipindi hicho.
Mioyo ya wana Simba na Watanzania kwa ujumla ilipata simanzi zaidi dakika za lala salama ambapo Berkane walisawazisha bao hilo, hiyo ikimaanisha Simba sasa walipaswa kupata magoli matatu zaidi, jambo ambalo halikuwezekana kwani muda haukuwa upande wao.
Kufuatia matokeo hayo, Berkane wametawazwa mabingwa wa msimu huu wa kombe la shirikosho la kandanda Afrika, ikiwa ni mara yao ya tatu kulitwaa, huku Simba ikiwa ni mara yao ya pili kupoteza mechi ya fainali, baada ya kufanya hivyo miaka 33 iliyopita walipopoteza dhidi ya Stela Abidjan katika michuano ya kombe la Washindi enzi hizo.
Aidha, hii ilikuwa mara ua pili kwa miamba hao wa soka nchini kupoteza fainali mbele ya mgeni rasmi kutoka familia ya Mwinyi, ambapo mwaka 1003 wakati wanapoteza fainali ya kwanza, mgeni rasmi alikuwa aliyekuwa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati huo Hayati Mzee Ally Hassan Mwinyi, na katika pambano la leo, mwanae Dkt Hussein Mwinyi ambaye ni raisi wa Zanzibar, alikuwa mgeni rasmi wa mechi.
Jambo jingine takiwa kuMiamba ya soka nchini Simba Sports Club,