Tuesday, June 17, 2025
spot_img

Watanzania wahimizwa kuchangia damu

Watanzania wameshauriwa kushiriki zoezi la kuchangia damu kusaidia kuokoa maisha ya wengine, hasa wagonjwa wa ajali, mama wajawazito, watoto wachanga, wagonjwa saratani na ukimwi wanaohitaji damu mara kwa mara.

Wito huo umetolewa leo Aprili 9,2025, na Mkurugenzi Mtendaji wa Kitengo cha Biashara wa Kampuni ya Simu ya Haloteli, Abdallah Salum wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu kwa kushirikiana na Kitengo cha Damu Salama Mkoa wa Dar es Salaam.

“Tunafurahi sana kuzindua kampeni hii muhimu ya kuchangia damu. Kama kampuni inayojali jamii, tunajivunia kuwa sehemu ya juhudi za kuokoa maisha na kuboresha afya za watu hivyo tunahamasisha ninyi kama jamii, wafanyakazi, na wateja wetu kushiriki kwa wingi ilikuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wengine,”amesema Salum.

Ameongeza ,”Kampeni hii itafanyika katika vyuo mbalimbali jijini Dar es Salaam,kwa kuhusisha huduma mbalimbali kutoka Halotel, ikiwa ni pamoja na mawasiliano, huduma za intaneti, na HaloPesa ili kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kuchangia damu.”

Salum amesema kampuni hiyo kwa kushirikiana na kitengo cha damu salama mkoa itaendeleza dhamira yake ya kuwa karibu zaidi na jamii kwa kuhakikisha upatikanaji wa damu salama katika hospitali na vituo vya afya nchini, sambamba na kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa uchangiaji damu wa mara kwa mara.

Ofisa uhamasishaji kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki,Joel Temba amesema wamelenga kukusanya damu chupa 500 kutoka kwenye Vyuo vikuu na vya kati vilivyochaguliwa na Kampuni ya Halotel ilikuokoa maisha ya mama na mtoto katika hospitali zote.

“Nashukuru hamasa imeenda vizuri kwani watu wamejitokeza kwa wingi kutoa damu hivyo wito wangu kwa jamii na vijana kuwa mabalozi wazuri kwa kutoa elimu ili kuwekeza katika benki ya damu kwani hakuna kisima cha damu kinachoweza kusaidia wenye huitaji huo bali sisi tena kwa kujitolea,”amesema.

Mwakili kutoka Kituo cha Sayansi Shirikishi Muhimbili( MUHAS), kitengo cha seli mundu, Dk Hilda Tutuba,ameihasa jamii kuendelea kuchangia damu ilikusaidia wagonjwa hao kwani matibabu yake yanahitaji damu nyingi iliwaweze kuokoa maisha yao.Mkazi wa Boko Wilaya ya Kinondoni,mkoa wa Dar es salaam, Martine Andai ameishukuru kampuni hiyo kwa kuandaa kampeni hiyo kwani itasaidia kuokoa maisha ya watu wengi zaidi nchini.

“Suala hili ni la kiroho kwani unapotoa damu kuokoa maisha ya watu wengine basi umefanya tendo kubwa la huruma kwa wenye huitaji na hii ni azina mbinguni hivyo jamii isiwe nyuma kwenye mambo ya muhimu kama haya ilikumuokoa mama na mtoto pamoja na watu wengine,”amesema.

Kauli mbinu ya kampeni hiyo ni ‘usalama wa mama na mtoto ni jukumu letu sote,changia damu okoa maisha’

Zinazihusiana

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Ungana Nasi Kupitia

0FansLike
0FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Za hivi karibuni