SHIRIKA la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, imesema idadi ya watu walionyongwa mwaka jana imeongezeka huku Iran, Iraq, na Saudi Arabia zikitajwa kuongoza katika kutekeleza adhabu hiyo.
Taarifa ya kila mwaka inaonyesha kuwa jumla ya watu 1,518 walinyongwa duniani kote mwaka 2024, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 32 kutoka mwaka 2023.
Katibu Mkuu wa Shirika la Amnesty International , Agnes Callamard, amesema utekelezaji wa adhabu ya kifo ni kukiuka haki za msingi za binadamu ambao haukubaliki kwa miaka ya sasa
Katika takwimu hizi Amnesty International ilishindwa kujumuisha maelfu ya watu walionyongwa nchini China ambao wanadaiwa kuongoza kutekeleza adhabu ya kifo
Katika ripoti hiyo, Iran imenyonga watu 972, wakati Saudi Arabia iliongeza idadi ya watu waliowanyonga kwa kuwakata vichwa kutoka 172 hadi karibu 345, na Iraq nayo ikiongezeka kutoka 16 hadi 63.